Jamani jamani jamani! hivi hii hali itaisha lini? Hivi ni nani wa kulaumiwa katika hili?
Kituo cha daladala Ubungo.
Hapa ni sehemu ambayo daladala nyingi ziendazo sehemu mbalimbali za nje na ndani ya jiji la Dar es Salaam zinapoanzia safari yake. Watu huchukua usafiri wa kuelekea waendako toka hapa na hakuna kati yao atakayejua nini kitatokea ndani ya usafiri (Daladala) aliouchukua. Jamani ndani ya Daladala kuna mengi mno, kati ya hayo yapo mazuri kwa maana watu tofauti hupata nafasi ya kujadili na mada tofauti zihusuzo jamii na mbalimbali yanayowazunguka. HILI ni moja kati ya mambo mazuri.
Daladala aina ya DCM ikitokea Mbagara kuelekea Kivukoni.
Jambo baya huwa ni pale ambapo mmoja kati ya abiria waliopanda ndani ya daladala hilo anapoamua kuonesha kipaji chake cha kucheza na mifuko ya abiria wengine kana kwamba ana ruhusa ya kufanya hivyo. Usipokua makini utajikuta hata ile nauli uliyotegemea kulipia usafiri huo imechukuliwa na Abiria huyu asiye na wema hata theluthi (KIBAKA).
Abiria wakiwa wamejaa kwenye DCM huku wengine wakiwa wamesimama katika style wanayoiita 'KUPIGA RANGI'
Kutokana na utofauti wa binadamu katika kukidhi haja zao, kila mmoja na njia tofauti na mwingine katika hili. Kuna watu ambao hupanda madaladala si kwa nia ya kuwahi kazini au kuiba kitu cha mtu mwingine La, Hasha! Wao hupanda Daladala na hasa zilizojaa tu ili waweze kujipa burudani ya KIMWILI. Watu hawa ni maarufu sana kwa jina la 'DUNGADUNGA'
Leo nimepata MOOD ya kuyaandika haya ili kuwatahadharisha watu hasa akina dada juu ya hawa watu. Haya yametokea leo wakti nikitokea nyumbani kwangu kuelekea kazini. Kuna njemba moja almanusura aambulie Kichapo kwa sababu ya kucheza KIDUKU nyumba ya mgongo wa dada fulani aliyekuwemo kwenye daladala tuliyoipanda. Jamaa huyo mtanashati ambaye kwa sura ni mzuri na angeweza kumnasa msichana yeyote ambaye angemtaka ameshindwa kufanya hivyo badala yake ameamua kuwa anamalizia shida zake kwenye madaladala yaliyojaa.
Kisa kilikua kama ifuatavyo: Jamaa amepanda kwenye gari kwa kuikimbilia kwa sababu tayari ilikuwa imeshajaa na abiriria wengi walikua wamesimama. Kwa mwendo wa kutoka Banana hadi maeneo ya TAZARA jamaa alionekana akicheza viduku taratibu kwa kumfuata dada wa watu kila hatua aliyosogea. Kumbe kitendo kile kilishuhudiwa vyema na Kondakta wa daladala hiyo ambaye aliamua kunyamaza kimya, (SIKUJUA aliogopa nini). Mbali na kondakta kuna jamaa mwingine ambaye pia alipata bahati ya kuliona hilo lakini alishindwa kuvimilia na kujikuta akimhoji jamaa kwa ukali kuwa alikuwa anataka nini kwa dada huyo (MDUNGWAJI). Jamaa kwa kujiuma uma alijibu kitu ambacho hakikueleweka kitu ambacho kiliamsha hisia za watu karibu wote kwenye daladala hiyo pamoja yule dada (MDUNGWAJI) mwenyewe ambaye kwa mara ya kwanza alisikika akisema, "mi nimemuona muda mrefu akinifuata fuata huku nyuma ila sikujua alikua anafuata nini", alisema dada huyo huku akiendele kuwa baada ya ahapo alisikia kama aliyeloana sehemu zake za MCHINA. Maneno ya dada huyu yaliamsha hisia za Abiria wengine ambao wengine walimuomba kondakta amlete Jamaa huyo (MDUNGAJI) huku nyuma (tulipokuwa tumekaa sisi) ili naye ADUNGWE.
Kwa bahati nzuri kabla ya maamuzi hayo kufikia muafaka jamaa alishuka maeneo ya MTAVA na kupanda daladala jingine ambayo hatukujua kama aliendelea na VIDUKU ama alikoma.
JAMANI mbona mademu wako wengi VIDUKU kwenye daladala vya nini?


