Nikiwa kama mzazi mwenye upendo wa dhati kwa mtoto wangu, nina kila sababu ya kukosa raha kutokana na matatizo haya yaliyomkuta mwanangu Rahmaritah. Si mimi tu bali hata mama yake pia hakuwa na raha hata kidogo.
Ni jambo ambalo lilimkumbusha mbali sana mama yangu Bi. Habiba na kusema kuwa kuna nyingi ya tabia na mambo yamtokeayo binti yangu huyu yanayoshabihiana na tabia ama mambo yaliyowahi kunitokea mimi katika makuzi yangu.
Hili ni Mojawapo.
Rahmaritah akiwa usingizini asubuhi ya siku ya pili baada ya tukio la kuungua na uji na kumsababisha kukosa usingizi usiku kucha kwa sababu ya maumivu makali aliyoyapata.
Katikahistoria ya maisha yake naye ameshaandika kuwa aliwahi kuungua na UJI.
Hii ni sehemu ya mkono wake iliyoungua kwa uji na kuichuna kwa kutumia nguo na kutoa gamba la juu la ngozi yake. INATISHA.
Baada ya kuamka siku ya pili yake na kuamua kunizuia nisiende kazini ili nishinde naye mchana kutwa. kwakweli kama ningekuwa nafanya kazi binafsi nisingetoka siku hiyo kwani nilikuwa nimejawa na usingizi na pia nilikuwa natamani kukaa naye ili nihakikishe hapati matatizo yoyote.
Miaka kadhaa ioiyopita mkono wangu huo niliouweka shavuni ulipata masahibu kama haya aliyoyapata binti yangu.
Lyk fadha lyk doughter.
Mungu msaidie Mwanangu apone haraka. AMIN